
CLOUDS MEDIA GROUP YAZINDUA MSIMU WA MALKIA WA NGUVU 2025 KWA KAULI MBIU “TWENDE DUNIANI”
Dar es Salaam, Machi 12, 2025 – Clouds Media Group imezindua rasmi msimu wa Malkia wa Nguvu 2025 kwa kauli mbiu Twende Duniani, ikiwa ni hatua kubwa katika kuwawezesha wanawake wa Tanzania.
Mwaka huu, Jukwaa la Malkia wa nguvu litafikia Kanda tano kuu Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kati, Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Kaskazini, na Kanda ya Pwani ukilenga kuwafikia zaidi ya wanawake 15,000 kupitia mafunzo, maonyesho ya biashara, na uwezeshaji wa kifedha.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga, alieleza dhamira yake ya miaka 30 iliyopita ya kujenga jukwaa maalum kwa wanawake. “Safari hii ilianza na mwanamke mjasiriamali, Mwanamakuka. Tuliona fursa na tukaiendeleza. Leo, tunasherehekea ndoto hiyo.”

Mwenyekiti wa Malkia wa Nguvu, Liliane Masuka, alieleza nguzo nne kuu za mpango wa mwaka huu:
✅ Mafunzo kwa Ushindani wa Kimataifa – Kupitia Maarifa Camps na Tuyajenge Talks, wanawake watapata ujuzi wa kuhimili ushindani wa kimataifa, ikiwemo safari ya wanawake 100 kwenda China kwa mafunzo ya biashara na uongozi.

✅ Upanuzi wa Masoko – Kupitia Mai Shop na Malkia Expo, wanawake wataunganishwa na masoko ya kikanda na kimataifa.
✅ Uwezeshaji wa Kifedha – Kupitia Kipepeo Seed Fund, wanawake vijana watapatiwa mitaji na mafunzo ya usimamizi wa fedha.
✅ Mtandao na Ushawishi – Kupitia Malkia wa Nguvu Gala & Awards, wanawake watapata fursa za kimataifa za kushirikiana na kubadilishana uzoefu.

Joseph Kusaga aliongeza kuwa Clouds Media Group imezindua Malkia Choice FM, redio ya kwanza inayotoa sauti kwa wanawake pekee, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha wanawake wanapata nafasi zaidi ya kusikika na kushiriki mijadala ya maendeleo.
Maadhimisho makubwa yatafanyika Aprili 4, 2025, katika The Super Dome, Dar es Salaam, ambapo Rais Samia Suluhu Hassan amealikwa rasmi kushiriki nasi katika siku hii adhimu.
All Categories
Recent Posts
CLOUDS MEDIA GROUP YAZINDUA MSIMU WA MALKIA WA NGUVU 2025 KWA KAULI MBIU “TWENDE DUNIANI”
Wafanyabiashara Watembelea Soko Kubwa la Fanicha na Vifaa mbalimbali Vya Mapambo – Foshan ,China
Wanawake Wafanyabiashara Chini ya TWCC Wawasili Nchini China.
+ 255 779 888 901
info@malkiawanguvu.co.tz