Tuzo za Malkia wa Nguvu zinazoendeshwa na Clouds Media Group zimehitimishwa usiku wa Novemba 29, 2024 Zanzibar kwa Malkia wa nguvu tisa kupewa tuzo kwenye sekta mbalimbali wanazohudumia mbele ya mgeni rasmi wa tuzo hizo; Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Mhandisi Zena Said ambaye amewataka wanaume kwenye maeneo mbalimbali kuwapa ushirikiano wake zao haswa wenye maono makubwa ya kiuchumi na kijamii.
1. Mama Mariam Mwinyi.
Tuzo ya Heshima imeenda kwa Mama Mariam, mke wa Rais wa Zanzibar, na muanzilishi wa taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF). ZMBF imewagusa wanawake wanaojishughulisha na uchumi wa buluu kwa makundi, na kuwapatia boti za kisasa zenye mashine, vifaa vya kazi, na tumaini jipya na kubadilisha taswira ya maisha yao.
2. Aisha Bakari Mohamed (Hijab Dj)
Yeye ameshinda tuzi ya sekta ya Burudani. Akiwa binti mdogo aliyezua gumzo kwa kuonekana DJ anayepiga muziki nila kuonesha maungo yake, yeye ni Hijab mwanzo mwisho. Kwa sas umaarufu wake siyo Zanzibar pakee, bali mpaka nje ya Zanzibar ambakohuoata mialiko ya kwenda kupiga muziki.
3. Mafunda Kombo Faki.
Ni mwanzilishi na mkurugenzi wa ZanVacay. Kupitia ZanVacay, siyo tu kwenye eneo la utalii linalohitaji kuongezewa thamani, ZanVacay imemtambulisha Mafunda katika ulimwengu wa kukutana na vijana, kutoa mafunzo mbalimbali yanayohusisha uongezaji wa thamani. pamoja na kuwa mmiliki wa ZanVacay, Mafunda ni mwajiriwa katika shirika la bima, na ni mshereheshaji katika matukio mbalimbali.
4. Saida Abdallah Mohamed.
Saida Abdallah Mohamed, mshindi wa tuzo ya Sekta ya Viwanda kupitia biashara ya viungo mbalimbali vya chakula, akiifanya kazi hii kwa miaka kumi sasa.
5. Bi. Fatma Eliah Masimba na Bi. Fatma Salum Abdallah
Sekta ya Ujasiriamali Bora, tuzo imeenda kwa watu wawili; Fatma Eliah Masimba na Fatma Salum Abdalah (Bi Sufa).
Binti Masimba alianza kuwa mhudumu wa mapokezi wa hoteli, baadaye akawa mmiliki mwakilishi, lakini kwa sasa ni mkurugenzi katika biashara kubwa ya familia yake. Akiwa mfanyakazi wa hoteli alikutana na mume wake ambaye amekuwa naye katika safari ya ujasiriamali na biashara, na kwa sasa anasimamia biashara mbalimbali ikiwa ni pamoja na vituo vya mafuta, ujenzi na usafirishaji.
Kwa upande wake Bi. Sufa, yeye aliozeshwa akiwa na miaka 14 mara baada ya kuhitimu elimu ya msingi, baadaye matokeo yalitoka akiwa amefaulu hivyo akaendelea na masomo. Alipomaliza shule, alianza maisha yake ya ujasiriamali na biashara nyingi katikati ya changamoto. Kutokana na maisha yake kutopata msingi mzuri wa kusoma, aliamua kuanzisha shule na kuziita Sufa Schools ambazo zipo kwa zaidi ya miongo miwili. Mbali na shule, yeye ni mmiliki wa ‘store’ kubwa ya vitu vya jumla, ‘fremu’ za kupangisha, na pia yeye ni mkulima mkubwa kutokana na mashamba aliyonayo.
6. Tatu Suleiman
Sekta ya Mitindo na Urembo mshindi ni Tatu Suleiman ambaye ameamua kuongeza thamani ya zao la mwani kwa kutengeneza vipodozi asili. Ni mwanzilishi wa bidhaa za Zaidat ambapo amefanikiwa kushika soko la ndani na nje ya Zanzibar.
7. Wanu Hafidhi Ameir
Ni mwanzilishi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation. Kupitia Mwanamke Initiatives Foundation, Wanu ameweka alama isiyofutika kwa kujali afya za wanawake, akiboresha huduma za afya ya uzazi na akili sambamba na kutoa mafunzo muhimu kwa wahudumu wa afya wa jamii. Kwa vijana, ameongoza njia mpya kwa kuwapa nafasi za mafunzo ya kiufundi na teknolojia.
8. Ramla Hamis Juma.
mkazi wa Pemba, ambaye ameshinda kwenye kipengele cha Biashara ya Chakula. Kwa sasa yeye ni mpishi mkubwa ambaye alianza kupika akiwa mtaani mpaka baadaye kuajiriwa Ikulu kama mpishi, lakini bado alikua na ndoto ya kusimamisha biashara yake mwenyewe, na amefanikiwa katika hilo, na kuweza kuajiri zaidi ya wafanyakazi 200.
Subscribe
We respect your privacy.
Join Malkia Wa Nguvu Family
Stay updated with all latest updates,upcoming events & much more.