Mkulima wa zao la mpunga kutoka Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, mpaka sasa ana ekari 275 na kuingiza sokoni tani 200 za mchele kila mwezi kiasi cha kuzalisha zaidi ya ajira 350.
2. SEKTA YA KILIMO ZAO LA MKAKATI
Joyce Romanus Mayemba.
Mjane na Mkulima wa zao la chai Mkoani Njombe anazalisha tani 300,000 kwa mwaka na kuzalisha zaidi ya ajira 250 kwenye mnyororo wa thamani.
3. MABORESHO SEKTA YA ELIMU
Dkt Miriam Elisha
Mwanzilishi wa kituo cha Elimu jumuishi cha watoto wenye usonji (autism) mkoani Iringa chenye watoto 35 na mpaka sasa kimeshatoa watoto 115 tangu kilipoanzishwa mwaka 2017 ambao wanasoma kwenye shule za kawaida.
4. INSPIRATIONAL ICON
Lightness Ndelwa
Mfanyabiashara kutoka mkoani Mbeya na mwanzilishi wa kwanza wa matamasha ya usiku wa mwanamke yaliyokuwa yakitoa mafunzo ya ujasiriamali na kufanikiwa kutoa mitaji kwa wanawake zaidi 1,000
5. UTUMISHI SEKTA YA UMA
Miriam Msalale
Katibu wa Afya na Afisa rasilimali watu wa hospitali ya kanda ya rufaa Mbeya na mwanzilishi wa kampeni ya matibabu ya figo kanda ya nyanda za juu kusini mwaka 2015. Miriam ameanzisha na kufanikisha mchakato wa ujenzi wa hospitali za rufaa katika mikoa ya Njombe na Katavi.
6. MAFANIKIO SEKTA YA BIASHARA
Blandina Mpangile
Mfanyabiashara kutoka mkoani Njombe mmiliki wa vituo vinne vya mafuta, viwanda vya mikanda ya gypsum Njombe na Dar es asalaam, kiwanda cha tofari na mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi aliyezalisha zaidi ya ajira 300.
Subscribe
We respect your privacy.
Join Malkia Wa Nguvu Family
Stay updated with all latest updates,upcoming events & much more.