Kabla sijapata tuzo nilikuwa nafanya biashara Mbeya pekee ila sasa nafanya biashara na mikoa yote nyanda za juu kusini na nimeongeza ajira kutoka vijana 100 hadi 230.
Nimeongeza idadi ya wateja na kufanukiwa kufungua duka linguine la nguo Kariakoo Dar es asalaam na sasa nafanya kazi nan chi za China, Uturuki na Malaysia.
Tangu nimepokea tuzo nimeongeza washirika wapya wa ndani kwenye biashara zangu, wapo walioniunga mkono na kuniongezea wigo wa kibiashara ndani na nje ya mipaka ikiwemo taasisi nyingi na mashirika kadhaa ya kijamii.
Imeniongezea umaarufu ndani ya jamii ambayo wengi walikuwa hawajui nafanya nini na sasa nimekuwa nikishiriki mijadala ya mabadiliko ya baadhi tamaduni kandamizi.