
Malkia Exposure Yawaongoza Wafanyabiashara Zaidi ya 50 Katika Safari ya Mafunzo na Ushawishi wa Kibiashara Nchini China



China Exposure Trip 2025
Mnamo 6 Septemba – 16 Septemba 2025, Malkia wa Nguvu iliongoza safari ya wafanyabiashara zaidi ya 50 kutoka Tanzania katika ziara ya kipekee nchini China.
Safari hii iliwapeleka washiriki katika miji ifuatayo:
- Guangzhou – kitovu cha maonesho ya kimataifa ya biashara na bidhaa.
- Yiwu – soko kubwa zaidi duniani la bidhaa ndogo ndogo na biashara ya jumla.
- Foshan – mji mashuhuri kwa viwanda vya samani, vifaa vya ujenzi na teknolojia ya nyumbani.
- Keqiao – maarufu kwa soko kubwa la nguo na vitambaa duniani.
Katika siku 10, washiriki walihudhuria maonesho ya biashara, walitembelea viwanda vikubwa, walijifunza kuhusu uvumbuzi wa kiteknolojia na uzalishaji, na kushiriki mijadala ya ushirikiano na wafanyabiashara wenzao wa China.
Athari na Mtazamo wa Baadaye
Malkia Exposure imekuwa daraja la mabadiliko kwa wafanyabiashara wa Tanzania. Kupitia uzoefu huu, washiriki wanatarajiwa kuendeleza miradi yao, kuongeza ajira, na kuchangia uchumi wa taifa kwa mtazamo wa kidunia.
Malkia wa Nguvu itaendelea kupanua programu hii kwa safari zaidi katika nchi mbalimbali, ikiendelea kuwafungulia Watanzania milango ya maarifa, mitandao na masoko ya kimataifa.
All Categories
Recent Posts
CLOUDS MEDIA GROUP YAZINDUA MSIMU WA MALKIA WA NGUVU 2025 KWA KAULI MBIU “TWENDE DUNIANI”
Wafanyabiashara Watembelea Soko Kubwa la Fanicha na Vifaa mbalimbali Vya Mapambo – Foshan ,China
+ 255 779 888 901
info@malkiawanguvu.co.tz