MALKIA WA NGUVU 7 WAPEWA TUZO KANDA YA KATI

Tuzo za Malkia wa Nguvu kanda ya Kati zimefanyika usiku wa tarehe 30/8/2024 Jijini Dodoma kwenye ukumbi wa Mabeyo Complex na kuwatunuku Malkia 7 wa Nguvu kutoka Mikoa mbalimbali inayowakilisha Kanda ya Kati.

Kwa miaka nane Clouds Media Group imekua ikiandaa na kuratibu tuzo za Malkia wa Nguvu kwenye sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Chakula, Mapambo, Utumishi wa Umma, Kilimo, Mwanamke mwenye ushawishi, Ustawi wa Jamii na Mjasiriamali bora.

Washindi wa tuzo hizo kwa Kanda ya kati ni pamoja na Raha Aloyce kwenye tuzo ya Kilimo Biashara, Happy Augustino (Near Me) sekta ya Biashara ya Chakula, Emeryciana Elikana Mbulagwisha (Ciana Event) Sekta ya Mapambo, Ntegenjwa Hosea Sekta ya Utumishi wa Umma, Mwalimu Sheila Hamis Chinja Mwanamke mwenye ushawishi, Ustawi wa Jamii Hilda Kalisa na Neema Shayo ambaye ameshinda tuzo ya Mjasiriamali Bora.

Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa amefurahishwa na hatua kubwa zilizopigwa na Clouds Media Group kwa kuhakikisha tuzo hizi zinafika Mikoani badala ya Dar es salaam pekee iliyokua ikifanyika miaka iliyopita.

Tuzo za Malkia wa Nguvu Kanda ya Kati zimehudhuriwa na watu mashuhuri mbalimbali akiwemo Mbunge wa Kusini Mashariki Babu Tale, Wabunge wa Viti Maalum Khadija Taya (Keisha), Nusrat Hanje, Catherine Magige, Mkurugenzi wa EFM na ETV Francis Cizar (Majizzo), Mtume Boniface Mwamposa na wengine wengi.

https://www.instagram.com/p/C_T7izMKw9j/?igsh=MW82Znh2aGoxcjNvaQ==

https://www.instagram.com/p/C_T7RxrisGt/?igsh=MWY3YWx0MHB0Y3d2cg==

https://www.instagram.com/p/C_Ti5DSqPWN/?igsh=aTd6Z3Z2YnUwdGR6

https://www.instagram.com/reel/C_Tg2c8N2mO/?igsh=MXVwenc0amI0c2s2OA==

https://www.instagram.com/reel/C_TgCDptoe1/?igsh=MXhwcWN6Y2liNmZ6cQ==

https://www.voiceofbongo.co.tz/2024/08/malkia-wa-nguvu-7-wapewa-tuzo-kanda-ya.html

Add a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe
SUBSCRIBE NOW

Join Malkia Wa Nguvu  Family 

Stay updated with all latest updates,upcoming events & much more.
close-link
Translate »