
Wanawake Wafanyabiashara Chini ya TWCC Wawasili Nchini China.



Wafanyabiashara wa Tanzania chini ya Mwavuli wa Chama cha wanawake wafanyabiashara Tanzania -TWCC Wawasili Nchini China Kushiriki Ziara ya Siku 10 ambayo inahusisha Kutembelea maonesho makubwa ya Canton Fair 2024, Kutembelea Viwanda vya kisekta, Kushiriki mikutano ya kimkakati na wawekezaji watarajiwa/potential investors, Kutembelea masoko ya vifaa mbalimbali n.k
Wafanyabiashara 77 wanashiriki maonesho ya Canton Fair wakitokea Tanzania ikiwa ni sehemu ya kujifunza teknolojia mbalimbali za uzalishaji. Msafara huu wa wafanyabiashara umeandaliwa na Chama cha wanawake wafanyabiashara Tanzania (TWCC) kuanzia Tarehe 15 hadi 27 Oktoba, 2024.
Tayari wafanyabaishara hawa wamewasili Nchini China na kufikia katika Mji wa Guangzhou ambapo leo katika siku ya kwanza ya ziara yao wametembelea maonesho ya Canton fair Phase I inayoanza tarehe 15 hadi 15 Oktoba, 2024.
Washiriki wametoka katika mikoa zaidi ya 20 nchini wakitokea katika sekta mbalimbali kama vile Ujenzi, kilimo, uvuvi, Uzalishaji, Utalii, Usafirishaji, Elimu, Viwanda kwa ujumla.
Ziara hii inatarajiwa kuwa ya mafanikio zaidi katika kipindi hiki ambacho mazingira ya biashara ni wezeshi na Wafanyabaishara/Wajasiriamali wa Tanzania wanatakiwa kujiimarisha ili kuweza kushindana katika masoko ya Kikanda na Kimataifa kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora pamoja na kuongeza uzalishaji.
All Categories
Recent Posts
CLOUDS MEDIA GROUP YAZINDUA MSIMU WA MALKIA WA NGUVU 2025 KWA KAULI MBIU “TWENDE DUNIANI”
Wafanyabiashara Watembelea Soko Kubwa la Fanicha na Vifaa mbalimbali Vya Mapambo – Foshan ,China
Wanawake Wafanyabiashara Chini ya TWCC Wawasili Nchini China.
+ 255 779 888 901
info@malkiawanguvu.co.tz