Usiku wa tarehe 27/7/2024 Jijini Arusha zimefanyika tuzo za Malkia wa Nguvu zilizoandaliwa na Clouds Media Group
Usiku wa tarehe 27/7/2024 Jijini Arusha zimefanyika tuzo za Malkia wa Nguvu zilizoandaliwa na Clouds Media Group kwa ajili ya Wanawake kwenye sekta mbalimbali kwa kutambua mchango wao mkubwa katika kujenga uchumi kuinua jamii iliyowazunguka.
Katika tuzo hizo Washindi ni Glory Silayo aliyeshinda tuzo ya uvumbuzi na ubunifu ambapo yeye kupitia kampuni yake anarejesha taka ngumu zinazotokana na glass na kuzifanya bidhaa ili kutumika tena, sekta ya madini Mshindi ni Lilian Rumisha yeye ni Mfanyakazi wa Chuo cha Madini Arusha, ni Mwalimu wa kukata mawe na amefanya kazi zaidi ya miaka tisa.
Sekta ya Mjasiriamali mshindi aliyetangazwa ni Linda Loleli mmiliki wa Garage ya Inda Car Service, sekta ya viwanda na biashara Mshindi ni Joyce Mmari ambapo ameeleza jinsi alivyoanza na bidhaa ya viungo na hivi sasa anamiliki kiwanda kikubwa na sehemu ya bidhaa zake anauza nje ya Nchi na alianza na House girl mmoja lakini sasa hivi ana mtaji wa milion 450 na Wafanyakazi 25.
Tuzo katika sekta ya mitindo na urembo Mshindi ni Upendo Matimati ni Manyabiashara wa bidhaa za manukato na anamiliki maduka zaidi ya matano alianza kwa kuuza urembo lakini aliajiriwa na baadaye aliacha kazi na kuanza biashara yake.
Sekta ya maendeleo ya biashara na chakula Mshindi ni Vick Lavicato yeye hivi sasa ameajiri Watu zaidi ya 200, tuzo ya mwisho ni ya sekta ya afya na ustawi wa jamii ambapo Getrude Kavishe ameshinda na kusema hivi sasa anamiliki Shule pamoja na Hospitali inayotoa huduma za kiafya.
Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Mh. Missaile Mussa, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, ameipongeza Clouds kwa tuzo hizo ambazo zina miaka nane tangu kuanzishwa kwake na wakati wa salaam za Mkoa wa Arusha amesema Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Paul Makonda kwa sasa yupo likizo.